Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gaddafi speaks Suaeli Kiswahili
VITEGA UCHUMI VYA DUNIA NA MAPITIO YA MAFUTA YAPO HATARINI
15.03.2008
Sera za Marekani ni hatari sana kwa marekani yenyewe na dunia,ni sera ambayo kauli mbiu yake(changu na cha maadui wangu).kanuni ya marekani yakusababisha madhara kwa wengine yameleta madhara kwa marekani pia,nahukumu zinazotolewa katika mahkama zakificho nakutokuwepo mtuhumiwa ,nakuhudhuria mawakili walarushwa ni silaha ya makali ya pande mbili huenda ikawa dhidi ya Marekani.
Uwekezaji wa dunia upo katika woga ,na mtaji upo katika woga pia,hivyo uekezaji utadumaa,fedha zitazorota,watakimbia kutumia dola ya marekani,usambazaji wa mafuta utasita kutokana nakikwazo cha mahkama za marekani,dola zitalinda fedha zaka dhidi ya mkono wa marekani endapo watazitoa nje ya nchi.
Mfano halisi wa hali hiyo ni pale Libya ilipotoa fedha zake kutoka soko la Marekani na washirika wake baada ya mgogoro wa Locarbe ,ikazirejesha ndani ikikhofia kudhibitiwa na marekani,mashirika ya petroli ya marekani yakaondoka na hasara,huenda yakafanya tena iwapo kanuni hiyo ya marekani itakaporejea..
Huenda Irani na Venezuela zikafanya vivyo kuondosha viekezaji vyake kutoka Benki za nje..huenda kukasitishwa usambazaji wa mafuta na kuuzwa nje,nkufungwa utumiaji wa dola ya marekani,hii itaitia hasara Marekani iliyokuja na sera hiyo.Mashirika ya Marekani yatakabiliwa na kutaifishwa na kufanywa ya ummah au kuchukuliwa nafasi yao na mashirika ya kichina.Na katika hali hii Marekani ndio yenye hasara,na hasa itakapoendeleza mwenenda huu nakuhalalisha kuweka mkono wake katika viwekezaji nje ya marekani.Na hii inamaanisha kuongeza spidi kwa nchi wekezaji kurejesha vitegauchumi vyake ndani ya nchi,japo kuvilinda tu iwapo marekani haitorekebisha sera zake mbovu.