Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gaddafi speaks Suaeli Kiswahili
KUIKEJELI URUSI
27.12.2008
Urusi ilikua ni lengo la Nchi za magharibi katika upanuzi wake kuelekea mashariki,na nguvu zote za kijeshi za magharibi zilielekezwa huko .mwanzoni mwa karne ya 19 "Nabilioni"aliziingilia nchi kadhaa za ulaya hadi Urusi iliyo tajiri wa mali asili za makaa ,chuma mafuta gesi na dhahabu...n.k. Nae Hitler katika vita ya pili ya dunia alivamia Urusi kwa lengo hilo hilo.
Leo Nato inafanya waliyoyafanya Nabilioni na Hitler kuelekea Urusi,ikatumia upenyo ulioachwa na kusambaratika muungano wa Urusi,nakutumia kile magharibi ilichokiita ushindi katika vita baridi dhidi ya kambi ya mashariki chini ya uongozi wa muungano wa sofieti,inajaribu kiasi iwezavyo kuziunganisha nchi zote zilizokuwa katika muungano huo kuanzia Asia ya kati,bahari nyeusi mpaka baltiki,baada yakuziunganisha nchi kadhaa zilizokua za kisoshalist ,hatua Urusi iliyoiona kuwa ni kukejeliwa na kufungwa pande zote,na hiyo ni ukweli mtupu ,kwani baada ya kusambaratishwa Ugoslavia na mnyororo uliopotea kukamilishwa ndani ya Nato hapo Urusi imezingirwa.
Urusi sio nguvu inayoweza kushindwa kirahisi,historia ya kale na sasa inatuonyesha hivyo,ni nchi iliyo na limbikizo la silaha za nuclear zipatazo vichwa vya nuclear 16000 ,zinaweza kurushwa kupitia ardhini na nyambizi na katika mizinga nyeti ambayo ni Urusi pekee inaimiliki duniani.sisi tunatoa wito tukitilia maanani amani ya dunia ili watu wasiingizwe katika mbahatisho mpya wa maangamizi.
Kuikejeli Urusi ni kuhatarisha amani ya dunia na tishio la vita vipya vya nuclear visivyo vya muhimu,hasa kwamba Marekani mara nyingi inategemea habari zisizo na ukweli na uchambuzi mbovu.
Hivi magharibi iliwaza kuwa madai ya uhuru wa Cosovo yatapelekea madai kama hayo kwa Abkhazia na Ositia ya kusini?!!na mchanganuo uliopelekea kuingia matatizo marekani nchini Iraq ulijengewa na taarifa za uongo zilizofikishwa na vibaraka waliokimbia nchi zao wakitarajia mapenzi ya makachero wa marekani.
Nato kuendelea kujipanua hakuna umuhimu wowote hasa baada ya Sofieti kusambaratika na kumalizika vita baridi,isipokua kama kuna nia yakuivamia Urusi na nchi nyengine duniani.
Marekani kama dola nyengine duniani ina haki ya kujilinda na kutaka iwe na amani daima,na pia eneo lake kijografia kati ya bahari ya atlantiki mashariki na na bahari ya pasifiki magharibi na kati ya bahari mgando kaskazini na dola ndogo za marekani ya kati na kusini zisiwe hatari kwa usalama wa taifa lake,iwe ni nchi iliyojaa amani kwa wahamiaji na wakimbizi, mbali na tamaa ya mabara ya kale, marekani ikiwa hivyo itastahiki kuwa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na Baraza la Amani ,likitizingatiwa ni dola iliyochangia maendeleo ya mataifa duniani nayo ni nchi isioegemea upande wowote.
Ama Marekani tulionayo leo,ni sehemu ya matatizo duniani na hivyo inatishia amani ya dunia na marekani yenyewe,Marekani lazima irejee kwenye " msingi wa Monro"Rais wa tano wa Marekani ( 1817-1825) : "kutojiingiza katika matatizo au mahusiano na ulaya na kutosaidia nchi za ulaya kupanua ukoloni wake kuelekea Marekani". Kuupanua msingi huu tunaongeza kutoingilia mambo ya nchi zote duniani.
Kama Ulaya ilivyo na haki ya kuwa na nguvu za kijeshi,kiuchumi na kisiasa na kuwa na jingo jipya lenye uwiano wa siasa za kimataifa.Iwachiwe Urusi nayo kama nguvu nyengine kihistoria inayopanda iwe huru wa kujenga nguvu ya uchumi kisiasa na kijeshi ili kujilinda.Ulaya inaweza kutojifunganisha na marekani iliyo mbali.na kuwa mbali kiunyeti na marekani na urusi.na bahari ya atlantiki iwe mbali kati ya marekani naulaya na kufaidika na mala asili za gesi na mafuta ya urusi.
Urusi ni mshirika kidemografia wa ulaya na sio marekani.laiti ulaya ingetathmini maslahi yake ingelijikaribisha na urusi na sio marekani,isipokua ikiwa ni msukumo wa kidamu au ukoloni wa marekani ulaya baada ya vita ya pili ya dunia!
Upumbavu na tama nakutokutathmini misimamo yatawaingiza watu katika maangamizi makubwa mara hii nahakuna ataeshinda kwani mapigano yatakua ni ya silaha za nuclear kati ya wenye kuzimiliki.
Dunia ijue urusi si ile muungano wa sofieti.kwani sofieti ilikua tawala iliyo na kaumu tofauti zilizoingizwa kwa nguvu katika muungano huo,na aidiolojia iliyodhihiri baadae kuwa watu hawakuiamini hata wakuu wa ceremlin pia.
Lakini Urusi ya leohaipiganii aidiolojia yakisiasa au kiuchumi au kifalsafa bali itatetea kaumu ya urusi na ummah wa urusi…nakuwepo kwa urusi,kwani ilipoanguka aidiliojia ya sofieti ya kimarkisia ummah haukuanguka,bali aidiolojia ndio ilioanguka,ummah wa sofieti upo palepale,bali ulipokea kuanguka kwake,uliobakia ni ummah ambao hautokubali kuanguka kwani kuanguka kwake ni kuanguka ummah..uhuru,uhai na uwepo wao,hii ni bora kifo kuliko kuishi hapana mjadala.
Kutozingatia yaliyotokea katika kupambana na muungano wa sofieti mwishe ni kujitia kitanzi…majiribio ya kale yaliyofanywa yatawaua wenyewe iwapo watayarejesha kwa urusi ya leo