Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili
Muammar Al Gaddafi speaks Suaeli Kiswahili
KIONGOZI AWAONGOZA MARAISI NA WAUMINI KUTOKA NCHI MALIMBALI DUNIANI MJINI KAMPALA KUADHIMISHA MAULIDI YA MTUME MUHAMMAD (SAW)
19.03..2008
Kiongozi ameanza kwa kuwaeleza waliohudhuria juu ya umuhimu wa maadhimisho hayo ya uzawa wa Mtume wa mwisho alieletwa kwa ajili ya watu wote tofauti na mitume wengine walioletwa kwa ajili ya watu au makabila yao tu,na Allah amesema (hakika ya dini inayokubalika na Allah ni dini ya kiislamu),akasema tena Allah (anaefuata dini isiokuwa ya kiislamu basi haitokubaliwa na akhera atakua miongoni mwa wenye kupata hasara),Qur ani ni kitabu pekee kitokacho kwa Allah hivi sasa ,sisi twaiamini Taurati na pia Injili,lakini Bible ya sasa sio ile aliyoiteremsha Allah kwa Issa,na Agano la kale si lile alyoteremshiwa Mussa,na ukweli wa Muhammad kuwa mtume wa mwisho ni kule kutajwa kwake katika Taurati na Injililakini injili na taurati za leo hazimtaji Muhammad,hii inamaanisha kuwa zimeghushiwa.
Mussa alisema atakuja mtume baada yangu jina lake Muhammad,na Issa aliwaambia banii Israili kuwa atakuja nabii baada yangu jina lake Ahmad.na Taurati au Injili yeyote haijataja jina la Muhammad imeghushiwa.
Issa katajwa mara "25" katika Qur ani,hatuwezi kufuta hata utajo mmoja wa Issa.
Mussa katajwa mara "138" katika Qur ani hatuwezi kufuta hata utajo mmoja .
Maryamu katajwa mara "38" ndani ya Qur ani.Yote ni kuwatukuza wajumbe hao,nasi tusipowaamini Mussa na Issa hatutokua waumini kwa sababu wametajwa katika Qur ani hivyo Qur ani ni kitabu kilicho sahihi hakijafutwa neon moja.
Ni juu yetu kuitafuta Taurati aliyoteremshiwa Mussa na Injili aliyoteremshiwa Issa.lakini zikowapi?!
Kwa bahati mbaya huenda kitabu kitakatifu kimetoweka na tulichonacho sasa kimeandikwa na watu na kufutwa yakufutwa.
Muhammad amezaliwa kwa kalenda ya jua tarehe 13-mwezi wa 4-kila mtu huuita mwaka "571"kwa kuukaribisha na mwaka wa uzawa wa Issa AS,ameishi miaka 63,yaani amekufa mwaka "634"kutoka kuzaliwa Issa A.S.
Leo tarehe tunayotumia ni ya uzawa wa Issa kwa sababu uzawa wake ulikua wa miujiza..ni alama ya Allah ..katika Qur ani umetajwa kwa urefu..Issa amezaliwa kwa upulizo kutoka kwa Allah bila ya Baba…ni miujiza..Issa kazungumza na watu akiwa mdogo..akiuhisha wafu kwa idhini ya Allah,akiponyesha wagonjwa kwa idhini ya Allah,akitengeza udongo katika umbo la ndege,akaupuliza na ukawa ndege kwa idhini ya Allah,akimuomba Allah ateremshe chakula kikateremshwa kutoka mbinguni kwa idhini ya Allah .ni miujiza inayopaswa tuiandike,imepita miaka miaka 2007,tangu miujiza hiyo kutokea.Lakini kuna tukio jingine inapaswa dunia iliandike nalo ni kufariki Muhammad juu yake amani,kwa nini?kwa sababu Muhammad ni mtume wa mwisho.ni tukio muhimu linalopaswa kuandikwa,kwani kifo che kimesitisha mawasiliano kati ya mbingu na ardhi..wahyi ulisita kabisa baada ya Muhammad,nahakuna mtume atakaekuja tena baada yake hadi kiama.
Ikwa uzawa wa Muhammad mwaka "571" au "570"baada ya uzawa wa Issa-hivyo tunaadhimisha leo tarehe 12 aliyozaliwa Muhammad S A W ni siku isiyo ya kawaida katika historia ya watu,ni siku aliyozaliwa na pia kufa baada ya miaka 63.asietumia tarehe hiyo ya uzawa wa Issa na kifo cha Muhammad mtume wa mwisho huyo ni mbaguzi na adui wa mitume ya Allah.na dunia isipotumia tarehe hii ni ile ya kibaguzi na chuki.ni mtume Issa mwenye miujiza na Mussa miujiza ya fimbo na kutia mkono katika kwapa lake ukatoka mwangaza.kuna vitabu vinazungumzia miujiza ya Muhammad kwa nini?kwa sababu kuna miujiza ya Mussa na Issa,wanasema vipi Muhammad hana miujiza ?Allah kataka hivyo.
Sisi tunamuamini Muhammad pasi na miujiza,anaetunga miujiza nakumsingizia Muhammad,huyo simuumini wa Muhammad.Muhammad inatosha kuwa kateremshiwa Qur ani ni tosha kuliko miujizo.ikwa huamini Qur ani bila miujiza hivyo hutokua muumini hata wa Qur ani..tosha kwa Muhammad kuwa mwisho wa mitume..hii haipo kwa mitume yote.
Katika Qur ani hakujatajwa Mtume na Malaika wa Allah isipokua Muhammad S A W..
Allah mtukufu na Malaika wake wanamtakia rehema Muhammad..mnasema amrehemu Muhammad kama alivyomrehemu Ibrahimu ni kosa kwani Ibrahimu hajasaliwa na Allah.maneno ya miujiza kadhaa ya Muhammad haina msingi kama kupasuka mwezi vipande viwili ,kulisha watu miamoja kibaba,kuchuruzika maji kutoka vidoleni mwake…yametoka wapi haya.?...yametoka kwa watu madhaifu wa imani.kwa sababu Mussa alipiga jiwe kwa fimbo yake nakutoka maji,wakadai kuwa hata Muhammad maji yalitoka katika vidole vyake jambo halijatokea.kwa nini Muhammad hajasema kwa nini sina miujiza ?..yeye anajua kama ni mtume na miujiza inamuhusu Allah nasio yeye.Muhammad ndio aliyetuelezea miujiza ya Mussa na issa baada ya kuambiwa kupitia wahyi.
Qur ani imemtaja Issa mara "25"..na pia imeitaja miujiza na Muhammad hawezi kubadilisha,na wala haoni chuki kwani miujiza ni ya Allah,naye anaiamini ..ni muumini wa alama ya Mussa na Issa naye ndio aliyetuambia kwni Jibrili amemuambia na kuandikwa kwenye mas hafu ambayo ni Qur ani.
Allah amempeleka Muhammad kutoka msikiti mtukufu kwenda msikiti wa al-aqsaa…huu ni muujiza wa kweli ,huu ni muujiza wa kweli uliotajwa katika Qur ani ..na Muhammad akaisimulia..hii inatosha sio kuongeza chumvi….kama wanavyofanya wengine katika tovuti jambo linalowateteresha watu.Mtume tunaeadhimisha uzawa wake leo hii ni wa watu wote,na wanaomuhujumu huko eskandanavia wanamuhujumu mtume aliyeletwa kwao pia,hao ni wajinga..ni wagonjwa..wanachuki..wabaguzi,dhidi ya ubinaadamu,dhidi ya Allah ,Mussa,Issa,kwani Issa amemuamini Muhammad,na Muhammad kamuamini Mussa na Issa.hivi waskendinavia wanamuamini Issa..?lahasha…ikiwa wanamuhujumu Muhammad hivyo wao ni Makafiri,wanamtukana mtume wa Allah..Allah atawaadhibu.
Wanadhani Muhammad ni mtume wa waarabu !Muhammad ni mtume wa waarabu na wasio waarabu nao hata wasitake ni mtume wao pia.Na Allah ameahidi ushindi wa dini ya Muhammad hata wakichukia washirikina na eskendanavia.
Allah anasema ni mtume asiejua kusoma wala kuandika yupo kwenye Taurati na Injili,lakini taurati na injili za sasa hukuti maneno haya.
Timbuktu tulizungumzia Hajji,iliyokuwepo wakati wa Muhammad..tokea Ibrahimu na Ismaili,yaani Makkah..Qaabah ilikuwepo kabla ya Ibrahimu na pia Ismaili ..kwa nini ?ili watu wahiji..watu gain ?siwale waliomuamini muhammad tu,bali hijja ilikua kabla ya Muhammad ni wajibu kwa watu wote,nasio waarabu au waislamu..ni wote kutoka Marekani..ulaya..australia..Asia ..Afrika ,kwa sababu Qaaba ni nyumba ya mwanzo aliyoijenga Allah ardhini.Ni ya watu wote ardhini wazunguuke Qaaba,watembee kati ya safaa na marwa,na wasimame katika jabali Arafaati.Allah anasema anaewazuia watu kuhiji katika Qaaba ,huyo ni kafiri tu..waarabu hawanahaki ya kuihodhi Qaabah.aya moja tu ndio inazuia washirikina kukaribia msikiti mtukufu hao ni uchafu,sasa akija Pop au rais wa marekani kwa uzoefu wetu tutamzuia akituuliza tuttafuta katika Qur ani tutakuta ayah ii,akituambia mmim sio mshirikina na sio mchafu,hivi mnaweza kumuambia wewe ni mshirikina na mchafu…sirahisi akisema mimi naamini Allah vipi uniambie hivyo?hapa kuna utata…haya ni kinyume na Qur ani.Awezae kwenda kwenye Qaaba aendeni ya watu wote na Allah alimuambia Ibrahimu awanadie watu hijja watakuja ktoka dunia nzima.
Maudhui ya mwisho muhimu kwa waislamu wote duniani ambao wengi wao wanabinywa nakufukuzwa na kukafirishwa..kuna makundi tuna wasunny na shia..na shia ni kundi.Nani asemae shia hawasumbuliwi ?wataktifu wanasumbuliwa..na kundi la shia linaandamwa kwa udhalimu na uadui ..ni kundi maarufu la kiislamu linasumbuliwa.linalonihusu mimi ni hali yakisiasa ya kundi hili..
shia ni raia wa ngazi ya pili nay a tatu katika nchi za kiarabu ..kwa kuwa shia anaandamwa sababu ni kuwa kwenye kundi la "ahlibaiti".
waliosemaAliniborakuwakiongoziwawaislamu..wamekuashia ALBAHRAHnikundilashialinaandamwakotedunia.,
ALBAHAIYYAHnalolinaandamwa
nakusumbuliwa,ALNAZARIAH,,,ALDURUZI,,ALNUSWAIRIAH,,ALZAIDIAH,,ALQADIANIA…yotehayanimakundi yakishia
..kwa sababu za kidini zimepelekea kukandamizwa makundi haya.Ukiwa shia ni mwiko kuwa raisi nchini humu au mfalme..na pia ukiwa sharifu kwani wanaungana na nyumba tukufu ya mtume.Hii ni hali ya kisiasa na sio ya kidini ni ukandamizaji wa haki za binaadamu ..
sisi ni watu kabla ya kuwa na dini..ni raia ndani ya nchi zetu kabla ya kuwa na mila.lazima tuwe sawa kisiasa ..taifa ni la wote. Hapa Uganda kuna kundi la ALBAHRAH wa ismailia wametoka India kutokana na kukandamizwa kisiasa,acha tofauti za kiitikadi kati yetu na Allah,ama kisiasa sote ni sawa.Mimi nipopamoja na wale wote wanaokandamizwa popote pale.hawa wanakandamizwa na kukimbilia nchi tofauti duniani kwa nini ?waacheni kati yao na Allah..wewe si Mungu wao,kutokana na ukandamizaji huo ndio tukatoa wito wa kuihuisha Dola ya Fatimia ya piliili kuwalinda hawa wanaokandamizwa .Dola hiyo itaanza kaskazini mwa Afrika hadi mashariki ya kati,laiti ingelisimama dola hiyo watajuta wale wanaowakandamiza makundi hayo wakati huo majuto hayatowafaidisha chochote.
Hawa wanyonge ipo siku itasimama dola yao…dola ya makadiani na bahaia,ismailia zaidia,bahra,shia,nuswairia na duruzi..
Ni swala linalogusa maisha yetu na si mjadala wakifalsafa au wa historia ya kale,la…twazungumzia hali ya kisiasa iliyopo.
Inshaallah tuuhishe siku hii kuu kizazi baada ya kizazimpaka dini ya Allah ishinde,nakuamini Muhammad ni mjumbe wa watu wote ,na dini ya kweli ni uislamu